Rais Xi asisitiza kusonga mbele kuelekea ushindi mpya wa usoshalisti wenye sifa maalumu za China
2022-09-28 08:40:01| CRI

Rais Xi Jinping wa China alisisitiza juhudi za pamoja kufanywa ili kusonga mbele kwa dhamira thabiti kuelekea ushindi mpya wa ujamaa wenye umaalumu wa China.

Rais Xi amesema hayo alipotembelea maonesho ya mafanikio yaliyopatikana kwa Chama na nchi katika muongo uliopita.

Rais Xi amesisitiza kuwa tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ufanyike mwaka 2012, Kamati Kuu ya Chama imeungana na kuongoza chama kizima, nchi na watu wake kutatua matatizo mbalimbali ambayo yalikuwa kwenye ajenda kwa muda mrefu lakini hayakutatuliwa, kutimiza mafanikio mengi yanayohusiana na mustakbali wa nchi, na kufanikiwa kukabiliana na hatari, changamoto na majaribu mengi ya kisiasa, kiuchumi, kiitikadi na kiasili.

Rais Xi ameongeza kuwa mafanikio na mabadiliko ya kihistoria yametokea kwenye shughuli kuu ya Chama na nchi, na kuiwezesha nchi kuwa na taasisi bora, misingi imara zaidi ya kiraslimali, na mawazo ya kujituma zaidi kwa ajili ya kutimiza ustawishwaji wa taifa.