Siku ya taifa ya China yasherehekewa nchini Ethiopia, mwito watolewa kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili
2022-09-28 08:55:25| CRI

Sherehe maalum ya kuadhimisha miaka 73 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China imefanyika mjini Addis Ababa Ethiopia.

Sherehe hiyo iliyofanyika kwa njia ya video na watu kukusanysika ukumbini imewaleta pamoja maofisa waandamizi wa serikali ya Ethiopia, wanadiplomasia wa China, wawakilishi wa jumuiya ya wafanyabiashara wa China na wanataaluma.

Akihutubia sherehe hiyo, aliyekuwa Rais wa Ethiopia Mulato Teshome amesema tangu China mpya ilipozaliwa uchumi wake umekua na kuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani. Amesema mafanikio ya China yametokana na uchapa kazi, busara na ujasiri.

Balozi wa China nchini Ethiopia Bw. Zhao Zhiyuan ameutaja uhusiano kati ya China na Ethiopia kuwa ni mfano wa kuigwa wa uhusiano kati ya China na Afrika, na kwamba uhusiano huo una mwelekeo mzuri.