Mjumbe wa UM asisitiza haja kwa jumuiya ya kimataifa kuwasiliana na Taliban wa Afghanistan
2022-09-28 08:39:20| CRI

Naibu mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Markus Potzel, amesisitiza haja kwa jumuiya ya kimataifa kuwasiliana na kundi la Taliban la Afghanistan.

Bw. Potzel ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kama Taliban hawaitikii mahitaji ya jamii ya waafghanistan na kuwasiliana kwa njia ya kiujenzi na jumuiya ya kimataifa, haijulikani ni nini kitafuata.

Ameonya kuwa hali inayozidi kuwa mbaya kama vile mgawanyiko, utengano, umaskini na mgogoro wa ndani, inaweza kusababisha uhamiaji mkubwa wa watu na kuweka mazingira yanayofaa kwa makundi ya kigaidi, na kuleta maumivu makubwa zaidi kwa watu wa Afghanistan.