Marais wa China na Argentina watumiana barua za kupongeza kongamano la ngazi ya juu la mawasiliano ya watu kati ya nchi zao
2022-09-28 21:38:24| CRI

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Argentina Alberto Fernández leo tarehe 28 walitumiana barua za pongezi kwa kongamano la ngazi ya juu la China na Argentina kuhusu mawasiliano kati ya watu na watu.

Rais Xi Jinping alifahamisha kuwa China na Argentina ni marafiki wakubwa na washirika wazuri. Huu ni mwaka wa 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Argentina, na pia ni mwaka wa ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizi mbili. Katika kipindi cha nusu karne iliyopita, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeshinda majaribu ya mabadiliko ya hali ya kimataifa, na kuwa mfano wa mshikamano, ushirikiano na maendeleo ya pamoja kati ya nchi zinazoibukia sokoni na nchi zinazoendelea. Maendeleo ya kina na ya haraka ya uhusiano kati ya China na Argentina ni mfano wa maendeleo makubwa ya uhusiano wa China na Amerika ya Kusini. Inatarajiwa kwamba wageni washiriki watajadiliana na kujenga maelewano ili kusaidia kuandika sura mpya katika ushirikiano wa kimkakati wa kina wa China na Argentina na kuchangia katika ujenzi wa jumuiya ya China na Amerika ya Kusini yenye mustakabali wa pamoja na jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu katika enzi mpya.

Katika barua yake ya pongezi, Fernandez alisema kuwa Argentina na China zimeshirikiana kwa nusu karne na zinaamini kwa dhati kwamba pande hizo mbili zitakuwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja na kiwango cha juu cha maendeleo. Ushirikiano wa kunufaishana kati ya vyombo vya habari vya nchi hizo mbili umekuza maelewano kati ya nchi hizi mbili. Inatarajiwa kwamba vyombo vya habari vitakuza ushirikiano, kuchangia katika ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya Argentina na China, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ustawi na neema ya watu wa nchi hizi pamoja na amani na maendeleo ya dunia.

Kongamano la ngazi ya juu kati ya China na Argentina kuhusu mawasiliano kati ya watu na watu lilifanyika tarehe 28 mjini Beijing, chini ya kauli mbiu ya "kukuza mawasiliano ya vyombo vya habari na kutafuta ustawi wa watu". Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na Sekretarieti ya vyombo vya habari na mawasiliano ya umma ya taifa la Argentina.