Zambia na China zafanya mkutano wa kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji
2022-09-29 09:29:53| CRI

Mkutano wa kwanza wa uwekezaji kati ya Zambia na China umefunguliwa mjini Lusaka ambapo nchi hizo mbili zimeahidi kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati yao. Rais wa Zambia Hakainde Hichilema na balozi wa China nchini Zambia Du Xiaohui walihudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

Balozi Du amesema lengo la mkutano huo ni kujenga jukwaa jipya la kutafuta uwezekano mpya wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Pia amesema nchi hizo zinatakiwa kuhimiza hali ya kuaminiana kisiasa na kushikilia usawa na haki ya kimataifa.

Rais Hichilema amesema China ni mshirika mkuu wa Zambia katika sekta ya biashara, kuongezeka kwa uwekezaji kutoka China hakika kunakaribishwa, na pia ameahidi kuwa serikali ya Zambia itaendelea kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji nchini humo.

Kampuni zaidi ya 300 za China na Zambia zimehudhuria mkutano huo wa siku mbili, huku nyingine 90 zikihudhuria kwa njia ya mtandao.