Ethiopia yasema mapendekezo ya China yataunga mkono mshikamano na amani
2022-09-29 09:08:02| CRI

Waziri wa fedha wa Ethiopia Bw. Ahmed Shide amesema pendekezo la maendeleo ya dunia na pendekezo la usalama duniani yaliyotolewa na China, yataunga mkono mshikamano na amani, wakati dunia ikielekea kwenye ushirikiano mkubwa na maendeleo.

Bw. Shide amesema Ethiopia inaunuga mkono mapendekezo hayo, na utayari wake wa kushirikiana na China kutekeleza mapendekezo hayo ni ushahidi kuhusu ushirikiano kati ya pande mbili kwenye jukwaa la kimataifa. Bw. Shide amesema hayo akihutubia sherehe ya miaka 73 ya siku ya taifa ya China iliyofanyika mjini Addis Ababa.

Bw. Shide amehakikisha kuwa serikali ya Ethiopia ina nia thabiti ya kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii na China, na ina matarajio ya kufanya ushirikiano huo ufikie ngazi ya juu zaidi katika miaka mitano ijayo.