Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amesema, hakuna yeyote mwenye haki ya kupigia kura ya turufu masuala yanayohusu hatma ya wapalestina.
Akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama, balozi Zhang Jun amesisitiza umuhimu wa kutetea haki kwenye suala la Palestina, na kulitaka baraza hilo kutekeleza majukumu yake bila upendeleo kwa mujibu wa mwafaka wa kimataifa na kuhimiza kurejeshwa mara moja kwa mazungumzo kati ya Palestina na Israel, badala ya kusubiri eti “hali mwafaka” ya mazungumzo kupevuka.
Balozi Zhang amesema, suluhisho la kudumu kwa suala la Palestina na Israel linatakiwa kuwa kwenye msingi wa ufumbuzi wa nchi mbili, ambao ni mwafaka wa kimataifa na mstari wa mwisho wa haki na usawa.