Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa lajadili matokeo mabaya ya ukoloni
2022-09-29 09:07:24| CRI

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limefanya mjadala kuhusu kasumba ya ukoloni kwenye maswala ya haki za binadamu.

Baraza hilo limesema kushughulikia kasumba hiyo kunaweza kuchangia kuondoa tofauti, na hata kuondoa changamoto za kutimiza maendeleo endelevu katika karne ya 21.

Mwenyekiti wa kamati ya kuondoa ubaguzi wa rangi ya Umoja wa Mataifa Verene Shepherd, amesema uhuru wa kisiasa na juhudi za kuondoa ukoloni havina maana kuwa ukoloni umeondolewa. Amesema kiwango ambacho nchi zilizokuwa makoloni zinaweza kufurahia uhuru wa kiuchumi na kijamii, kinakwamishwa na kasumba ya ukoloni, hasa ukuu wa wazungu.

Ofisa anayeshughulikia hali ya sasa ya ubaguzi wa rangi, kikabila na kukosa uvumilivu Bw. Jose Tzay, amesisitiza haja ya kutambua haki za wazawa kujiamulia mambo.