Waziri mkuu wa China apongeza kuzinduliwa kwa Faharisi ya Uvumbuzi Duniani 2022
2022-09-30 09:16:40| CRI

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametuma barua ya pongezi kwa Shirika la Hakimiliki Duniani (WIPO) kutokana na kuzinduliwa kwa Faharisi ya Uvumbuzi Duniani (GII) ya mwaka 2022.  

Kwenye barua yake Bw. Li ameutaja uvumbuzi wa sayansi na teknolojia kuwa ni msukumo mkubwa kwa maendeleo ya jamii ya binadamu, na kusema China imeweka umuhimu mkubwa katika uvumbuzi, imejitahidi kujiunga na mtandao wa uvumbuzi duniani, kulinda hakimiliki na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kuhusu uvumbuzi wa sayansi na teknolojia kwenye nyanja zote.

Kwa mujibu wa orodha mpya ya nafasi za nchi kwa faharisi ya uvumbuzi iliyotolewa jana na WIPO, nafasi ya China imepanda kutoka 34 ya miaka kumi iliyopita hadi kufikia 11 mwaka huu, na kuendelea kuwa nchi pekee yenye kipato cha kati kwenye nafasi 30 za mwanzo.