Jeshi la Somalia laangamiza magaidi 40 wa al-Shabab katikati mwa nchi
2022-09-30 09:31:52| CRI

Shirika la habari la Somalia limesema jeshi la Somalia (SNA) limewaangamiza magaidi 40 wa kundi la al-Shabab Alhamisi wiki hii huko eneo la Hiran, katikati mwa nchi hiyo.

Makamanda waandamizi wa jeshi hilo wamesema magaidi hao waliuawa katika mapigano makali yaliyotokea katika kijiji cha Ceel-Qooxle na sasa wanaendelea kuwasaka wengine waliokimbia.

Ceel-Qooxle ni kati ya vijiji kadhaa vilivyokombolewa katika operesheni za hivi karibuni kusini na katikati mwa Somalia, zilizotekelezwa na vikosi vya serikali na kienyeji, na kufanikiwa kulifurusha kundi la Al Shabaab kutoka kwenye ngome kadhaa lililoziteka kwa zaidi muongo mmoja.