China na Argentina zatoa mfano mzuri kwa mshikamano na ushirikiano wa nchi zinazoibukia kimasoko
2022-09-30 10:22:55| CRI

Rais Xi Jinping wa China tarehe 28 alituma barua ya pongezi kwenye kongamano la ngazi ya juu la China na Argentina kuhusu mawasiliano kati ya watu na watu, akitumai kongamano hilo litasaidia kufungua ukurasa mpya katika uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Argentina na kuchangia katika ujenzi wa jumuiya ya China na Amerika ya Kusini yenye mustakabali wa pamoja na jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu katika enzi mpya.

Naye Rais Alberto Fernández wa Argentina pia alituma barua ya pongezi kwenye kongamano hilo, akitarajia kuimarisha ushirikiano wa pande mbili, kuchangia katika uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya Argentina na China, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ustawi na neema ya watu wa nchi hizi pamoja na amani na maendeleo ya dunia.

Huu ni mwaka wa 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Argentina. Barua hizo za pongezi zinaonyesha kuwa marais wa nchi mbili wanatilia maanani ushirikiano wa China na Argentina katika enzi mpya, pia ni ishara ya kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Argentina, na kuhimiza ushirikiano wa mawasiliano ya kijamii. Katika miaka hii 50, uhusiano wa China na Argentina umekuwa wa wenzi wa kimkakati wa pande zote, ambao umewanufaisha watu wa nchi hizo mbili.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa mwezi Februari mwaka 2022 juu ya kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Argentina, Argentina ilisisitiza tena kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja, na China ilisisitiza tena kuiunga mkono Argentina katika kutekeleza kikamilifu mamlaka yake juu ya suala la visiwa ya Malvinas. Hatua hizo zimeimarisha urafiki kati ya China na Argentina.

Mbali na hayo, maendeleo ya uhusiano wa kibiashara kati ya China na Argentina yamewanufaisha watu wa nchi hizo mbili. Katika mwaka 2021, thamani ya biashara kati ya China na Argentina iliongezeka kwa asilimia 28.3 na kufikia dola bilioni 17.83 za kimarekani, ambapo China imeendelea kuwa mshirika wa pili wa biashara kwa Argentina. Februari mwaka huu, China na Argentina zilitia saini makubaliano zaidi ya kumi, ikiwa ni pamoja na kumbukumbu ya maelewano juu ya kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Kwa sasa, China na Argentina zinashughulikia kazi za ufufuaji wa uchumi kukabiliana na athari mbaya za janga la COVID-19 na kuwanufaisha zaidi watu. Nchi hizo mbili zinahimiza zaidi ushirikiano ili kukabiliana na changamato za kimaendeleo. Kwa mfano, China na Argentina zinajenga kwa pamoja kituo cha umeme wa nishati ya maji kwenye ukingo wa mto Santa Cruz, kituo ambacho kitaisaidia Argentina kupunguza gharama kubwa ya kuagiza mafuta kutoka nje.

China na Argentina zikiwa ni marafiki wa muda mrefu, kuwasiliana na kufundishana kati ya watu wa nchi mbili ni nguvu kubwa ya ushirikiano wa pande mbili. Vyombo vya habari vya nchi mbili vinafanya kazi muhimu kwenye sekta hiyo, na vinapaswa kueleza vizuri hadithi za kunufaishana, ili kulinda amani na maendeleo, kuhimiza ushirikiano wa biashara, kueneza urafiki kati ya pande mbili, na kuweka mazingira mazuri ya kimataifa yenye haki na ukweli kwenye sekta ya vyombo vya habari.