Rais wa China aweka mashada ya maua kuwakumbuka mashujaa katika Siku ya Mashujaa
2022-09-30 10:31:30| CRI

Leo tarehe 30, Septemba ni Siku ya Kuwakumbuka Mashujaa kwa mujibu wa sheria ya China. Rais Xi Jinping wa China pamoja na viongozi wengine wa Chama na serikali na wajumbe kutoka sekta mbalimbali za kijamii walishiriki kwenye  hafla hiyo iliyofanyika  kwenye Uwanja wa Tiananmen wa Beijing na kuweka mashada ya maua kwenye Mnara wa Kumbukumbu ya Mashujaa.