Vivutio vya utalii vyatangazwa kwenye maonesho ya utalii ya kimataifa ya Algeria
2022-09-30 09:16:04| CRI

Maonesho ya 21 ya Utalii na Safari ya Kimataifa yamefunguliwa mjini Algiers baada ya kusitishwa kwa miaka miwili kutokana na janga la Uviko-19.

Maonesho hayo yalizinduliwa na waziri mkuu wa Algeria Ayman Benabderrahmane pamoja na maofisa wa serikali na mabalozi wa nchi mbalimbali, Saudi Arabia ikiwa ni nchi mgeni wa heshima.

Kwenye maonesho hayo Banda la Ubalozi wa China limetangaza vivutio vya utalii vya China kwa watu wa Algeria kupitia picha, filamu, vipeperushi vya njia za utalii na postikadi za mandhari.

Bw. Benabderrahmane amewashukuru waonyeshaji wa China kuhudhuria maonesho hayo na kusema anatarajia watalii wengi zaidi kutoka China wataitembelea Algeria na kuimarisha zaidi uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili.