Jumuiya ya Afrika Mashariki yazihimiza nchi wanachama kujiandaa dhidi ya mlipuko wa Ebola Uganda
2022-09-30 09:53:42| CRI

Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC imezihimiza nchi wanachama kujiandaa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda.

Uganda ikiwa moja ya nchi saba wanachama wa jumuiya hiyo, Septemba 20 imetangaza mlipuko wa Ebola baada ya mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya Ebola aina ya Sudan kuthibitishwa katika sehemu ya Mubende iliyoko katikati ya nchi hiyo.

EAC imetoa taarifa kupitia makao makuu yake huko Arusha ikizihimiza nchi wanachama kuimarisha usimamizi na upimaji wa maabara, hasa katika maeneo ya mipaka. Sekretarieti ya EAC pia imezitaka nchi wanachama kutekeleza hatua sahihi za kukinga na kudhibiti maambukizi, na kuongeza elimu kuhusu hatari ya ugonjwa huo kwa jamii.