Rais Xi Jinping akutana na kundi la wataalamu wanaotengeneza ndege ya C919 na kuwapongeza kwa mafanikio
2022-10-01 22:04:04| cri

Rais Xi Jinping wa China amepongeza mafanikio yaliyopatikana katika uundaji wa ndege kubwa ya abiria ya C919, na kutoa wito wa mafanikio makubwa zaidi katika utengenezaji wa vifaa vya hali ya juu nchini China.

Rais Xi amesema hayo alipokutana na wawakilishi wa timu ya mradi wa C919 na kutazama maonyesho ya mafanikio ya mradi huo kwenye Ukumbi Mkuu wa mikutano ya umma wa Beijing.

Rais Xi amesema juhudi zinapaswa kufanywa ili kufikia mafanikio katika teknolojia muhimu na za msingi, na kuongeza kuwa usalama unatakiwa kuwa kipaumbele, na uundaji wa ndege hiyo kubwa utafanywa vizuri.

Alhamisi shirika la utengenezaji wa Ndege za Kibiashara la China, linalotengeneza ndege aina ya C919, lilipata cheti maana kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Ndege ya China.

Kutokana na mpango wake wa maendeleo ulioidhinishwa mwaka 2007 na safari yake ya kwanza ya mwaka wa 2017, C919 ni ndege ya kwanza ya China iliyotengenezwa kwa mujibu wa viwango vya kimataifa ikiwa na haki miliki za kujitegemea.