Kiongozi wa mapinduzi wa Burkina Faso asema hali imedhibitiwa
2022-10-03 10:11:54| CRI

Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi aliyejitangaza nchini Burkina Faso Kepteni Ibrahim Traore amesema kuwa hali imedhibitiwa na hali inarejea kuwa ya kawaida hatua kwa hatua, baada ya kutangaza kufukuzwa kwa rais Luteni Kanali Paul-Henri Sandago Damiba Ijumaa jioni.

Amewataka watu kuendelea na shughuli zao kwa uhuru na kujizuia kufanya vitendo vyovyote vya kuleta vurugu na uharibifu wa mali, hasa wale wanaoulenga ubalozi wa Ufaransa na kambi ya kijeshi ya Ufaransa ambayo imeripotiwa kumuhifadhi rais Paul-Henri Damiba, ambaye alipanga kufanya shambulizi la kujibu. Hata hivyo Ufaransa imekanusha kwamba kambi yake inamhifadhi Damiba baada ya kupinduliwa Ijumaa.

Jumamosi jioni, kupitia ukarasa wake wa Facebook, rais Paul-Henri Sandago Damiba alimtaka Kepteni Traore kuwa muelewa ili kepusha vita. Hadi sasa mahali alipo Damiba bado hapajulikani.