Wataalamu wa UM walaani vitendo vya ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika
2022-10-04 10:04:31| CRI

Wataalamu wa Kikosi Kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu mambo ya watu wenye asili ya Afrika jana walihutubia kwenye mkutano wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa wakisema, hali ya haki za binadamu ya watu wenye asili ya Afrika inahitaji kushughulikiwa haraka, kwani ubaguzi wa rangi bado unaendelea kutokea katika hali zote za maisha.

Wataalamu hao walieleza kukasirishwa na vurugu dhidi ya watu wenye asili ya Afrika kutokana na ubaguzi wa rangi. Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho Catherine S. Namakula alisema matumizi ya nguvu kupita kiasi na mauaji ya watu wenye asili ya Afrika yanayotekelezwa na idara za sheria hayajaadhibitiwa katika nchi nyingi.

Ameongeza kuwa kikosi chake Jumatatu kiliwasilisha ripoti mpya inayowafuatilia watoto wenye asili ya Afrika, akisisitiza kuwa historia halisi ya Afrika inapaswa kufundishwa ili kupambana na ubaguzi wa rangi.