Bunge la chini la Russia Duma laidhinisha makubaliano ya kuyaunga maeneo ya Donetsk, Lugansk, Zaporizhzhia na Kherson nchini Russia
2022-10-04 10:09:59| CRI

Baraza la chini la bunge la Russia Duma limeidhinisha makubaliano ya kuyaunga maeneo ya Donetsk, Lugansk, Zaporizhzhia na Kherson nchini Russia.

Kwa mujibu wa taarifa, wajumbe wa Baraza la Duma walipiga kura kwa kauli moja ya kuunga mkono sheria hiyo. Mwenyekiti wa Duma Vyacheslav Volodin alisema kufuatia upigaji kura huo, kujiunga na Russia ni njia ya kulinda haki za watu waishio katika maeneo haya. Amesisitiza kuwa malengo ya operesheni maalum ya kijeshi yameamuliwa, na yatafikiwa bila kushindwa.

Sherehe zilifanyika Ijumaa kwa ajili ya kusainiwa kwa mikataba ya kuzijumuisha Donetsk, Lugansk, Zaporizhzhia na Kherson katika Shirikisho la Russia.