Rais wa Uganda amwondoa kamanda wa vikosi vya ardhini kwenye nafasi yake baada ya kutoa kauli yenye utata
2022-10-05 09:44:27| CRI

Rais wa Uganda Yoweri Museveni jana alimuondoa kamanda wa Vikosi vya Ardhini Muhoozi Kainerugaba kwenye nafasi yake, baada ya kuandika kwenye Twitter kwamba jeshi lake linahitaji wiki mbili tu kuutia mikononi mji wa Nairobi.

Kwenye taarifa yake jeshi la Uganda limesema nafasi ya Kainerugaba ambaye pia ni mwana wa rais, itachukuliwa na Kayanja Muhanga ambaye amepandishwa na kuwa Luteni Generali. Muhanga alikuwa akiongoza mashambulizi dhidi ya vikosi hasimu mashariki mwa nchi jirani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa taarifa, Kainerugaba ataendelea kufanya kazi kwenye nafasi ya Mshauri Mwandamizi wa Rais kwenye Operesheni Maalumu.