Rais Zelensky wa Ukraine asaini amri ya kukataa mazungumzo na Putin
2022-10-05 09:40:54| CRI

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesaini amri ya kutekeleza uamuzi wa Baraza la Usalama na Ulinzi la Kitaifa (NSDC), ambao umefuta uwezekano wowote wa kufanya mazungumzo na Rais Vladimir Putin wa Russia.

Rais Zelensky pia aliiagiza serikali kuandaa mapendekezo ya kuundwa kwa mfumo wa ngazi mbalimbali wa kuhakikisha usalama kwa ajili ya kuongeza uwezo wa ulinzi wa Ukraine.

Septemba 30, Baraza la NSDC lilipitisha uamuzi unaolenga kulinda usalama wa Ukraine na kurejesha ukamilifu wa ardhi yake kufuatia Russia kutambua rasmi mikoa minne ya Ukraine, ambayo kwa kiasi fulani inadhibitiwa na Russia, kama eneo la Russia.