Mradi wa maendeleo ya kijani kando ya mto uliofadhiliwa na China wakabidhiwa kwa Ethiopia
2022-10-05 09:46:34| CRI

Awamu ya pili ya Mradi wa Maendeleo ya Kijani Kando ya Mto wa Addis Ababa uliofadhiliwa na China umekabidhiwa rasmi kwa serikali ya Ethiopia. Mradi huo unajumuisha jumba la makumbusho la sayansi na kiwanja cha kucheza watoto.

Balozi wa China nchini Ethiopia Bw. Zhao Zhiyuan alihutubia hafla ya kukabidhi mradi huo iliyofanyika Jumatatu akisema, mradi huo utahimiza maendeleo ya sayansi na teknolojia, na utakuwa sehemu nzuri ya kufanyia mikutano, mikusanyiko, harusi na shughuli kwa watoto. Ameongeza kuwa kukamilika na kukabidhiwa kwa mradi huo kunaonesha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote na urafiki mkubwa kati ya China na Ethiopia.

Mradi huo ulianza kujengwa mwezi Mei mwaka 2020, ikiongozwa na Pendekezo la Maendeleo Duniani na “Mipango Tisa” ya ushirikiano kati ya China na Afrika, China imekabiliana na changamoto zinazotokana na janga la Corona, na kukamilisha kazi zote kwa mafanikio.