Nchi za Afrika zaahirisha biashara ya hisa ya kuvuka mpaka hadi mwezi Desemba
2022-10-06 09:50:46| CRI

Ofisa mkuu mtendaji wa Bodi ya biashara ya hisa ya Nairobi Bw. Geoffrey Odundo amesema nchi za Afrika zimeahirisha biashara ya hisa ya kuvuka mpaka kutoka mwezi Oktoba hadi Desemba.

Odundo amesema Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itasaidia kuziunganisha bodi kumi za biashara ya hisa za Afrika kupitia jukwaa la kidigitali, jukwaa ambalo linawawezesha wawekezaji kununua moja kwa moja hisa na madeni ya nchi nyingine za Afrika kupitia madalali wenyeji wanaouza hisa.

Ameongeza kuwa Morocco, Ghana, Misri, Botswana, Kenya na Nigeria ni baadhi ya nchi zinazoshiriki kwenye mpango wa majaribio ya biashara ya kuvuka mpaka, mpango ambao utatekelezwa na sehemu nyingine za Afrika.