Walinda amani na vikosi vya serikali ya DRC wakabiliana na uvamizi wa waasi dhidi ya raia
2022-10-06 09:43:16| CRI

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokraia Kongo (MONUSCO) imetuma walinda amani huko Vido eneo la Beni mkoani Kivu Kaskazini, kuungana na vikosi vya jeshi la DRC ambako waasi wamevamia na kuwaua raia wanane siku ya Jumanne.

Akifafanua tukio hilo, Stephane Dujarric ambaye ni msemaji mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kumekuwa na ripoti kwamba waasi walichoma moto nyumba 10 na shule. Washambuliaji hao wanaaminika kutoka kundi la waasi la ADF. Amesema uvamizi huo umesababisha raia kuondoka kwenye makazi yao na kukimbilia eneo jirani la Tchabi na kwenye kambi za jeshi la serikali.