Serikali ya Ethiopia yaunga mkono mwaliko wa AU wa maongezi ya amani na waasi
2022-10-06 09:45:29| CRI

Serikali ya Ethiopia imesisitiza kwamba inaunga mkono mwaliko wa Umoja wa Afrika kwa ajili ya mazungumzo ya amani na waasi wa TPLF.

Kwenye taarifa kwa wanahabari, Idara ya Serikali inayoshughulikia Huduma ya Mawasiliano imesema vyombo vinavyoongoza mazungumzo ya amani ya AU vimetoa mwaliko wa mazungumzo hayo kuanza na kutangaza tarehe na eneo la kufanyia. Awali serikali ilieleza msimamo wake kwamba wapatanishi kwenye mazungumzo hayo ya amani ni lazima wawe AU pekee na yafanywe bila masharti yoyote.

Idara ya Serikali inayoshughulikia Huduma ya Mawasiliano imesema serikali kuu inaendelea na azma yake ya kutumia hatua zote zinazowezekana kutatua mgogoro kwa njia ambayo itahakikisha amani ya kudumu, ukamilifu wa ardhi na kusisitiza kuwa itaendelea kushikilia azma hii.