Kenya kupokea watalii wa kigeni milioni 1.46 mwaka 2022
2022-10-06 09:44:30| CRI

Kenya imekadiria kwamba itapokea watalii kutoka nje milioni 1.46 katika mwaka 2022, idadi ambayo itaongezeka kutoka laki 8.7 iliyorekodiwa mwaka jana, kufuatia kufufuka kwa uchumi baada ya janga la UVIKO-19.

Akiongea kwenye ufunguzi wa Maonesho ya 12 ya Utalii ya Magical nchini Kenya, Waziri wa Utalii na Wanyamapori Najib Balala amesema mapato ya sekta ya utalii yanatarajiwa kuongezeka kutoka dola za kimarekani bilioni 1.2 mwaka uliopita, hadi bilioni 2.19 mwaka huu. Amebainisha kuwa Kenya ikiwa eneo la utalii iko njiani kufufuka haraka kutokana na kuongeza thamani kwenye masuala ya utalii pamoja na kutoa mambo mbalimbali.

Balala amesema maonesho ya utalii, ambayo ni maonesho makubwa zaidi ya utalii katika Afrika Mashariki na Kati, yamewaleta pamoja waoneshaji 200 na wanunuzi 160 kutoka Ulaya, Afrika, Asia na Marekani. Utalii ni moja ya vyanzo vya fedha za kigeni nchini humo.