Majaribio ya kutumia masuala yanayohusiana na Xinjiang kuiangusha China hayatafika popote
2022-10-07 09:48:35| CRI

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema ukweli umethibitisha tena na tena kwamba kufanya suala la haki za binadamu kuwa la kisiasa na kutekeleza vigezo tofauti si mambo yanayopendwa na watu, na majaribio ya kutumia masuala yanayohusiana na Xinjiang kuiangusha au kuidhibiti China hayatafika popote.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, mkutano wa 51 wa Baraza la Haki za Binadamu, Oktoba 6 ulipiga kura ya kukataa rasimu ya uamuzi unaoongozwa na Marekani juu ya Xinjiang.

Wizara hiyo imesema kwa muda mrefu sasa, Marekani, na baadhi ya nchi za Magharibi zimekuwa zikiupotosha umma kuhusu Xinjiang na kutaka kufanya ghilba ya kisiasa kwa jina la haki za binadamu, ili tu kuchafua sifa ya China na kudhibiti maendeleo yake.

Amefafanua kuwa jamii ya kimataifa haiwezi kupotoshwa kirahisi, na kuongeza kuwa licha ya shinikizo la Marekani na nchi nyingine za magharibi dhidi ya nchi wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu, rasimu hiyo haikuungwa mkono na wajumbe wa Baraza hilo, hasa wajumbe wengi kutoka nchi zinazoendelea.