Wazalishaji wa Petroli barani Afrika waiunga mkono OPEC kupunguza uzalishaji wa petroli
2022-10-07 09:50:03| CRI

Shirika la Wazalishaji wa Petroli la Afrika (APPO) limetangaza kuunga mkono uamuzi wa Shirika la Nchi Zinazosafirisha Petroli kwa Wingi (OPEC) na baadhi ya nchi zinazozalisha petroli ambazo si za OPEC, kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa mapipa milioni mbili kwa siku kuanzia mwezi Novemba.

Omar Farouk Ibrahim, Katibu mkuu wa APPO amesema kwenye taarifa kwamba uamuzi huo umepokelewa vizuri na anaamini kuwa ni jambo sahihi kufanya ili kuokoa sekta na pia kuhakikisha kuna utulivu leo na kesho. Amefafanua kuwa kila nchi ina wajibu wa kulinda maslahi ya wananchi wake, na kama kwa kupunguza uzalishaji ndio itakuwa kutumikia maslahi yao bora, wacha iwe hivyo.

Kwa mujibu wa Farouk, mabadiliko hayo yamefanywa kutokana na hali isiyo na uhakika kwenye uchumi wa dunia na mtazamo wa soko la mafuta pamoja na mahitaji ya kuboresha mwongozo wa muda mrefu kwa soko la mafuta.