Mkutano wa saba wa Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China wafanyika
2022-10-09 14:57:44| cri

Mkutano wa saba wa Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefanyika jana jumapili mjini Beijing.

Katika mkutano huo, rais wa China Xi Jinping akiwakilisha Ofisi ya Siasa ya Kamati hiyo, alitoa ripoti ya kazi na maelezo juu ya rasimu ya ripoti iliyotolewa na Kamati Kuu ya 19 kwa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.

Wang Huning ametoa maelezo juu ya rasimu ya marekebisho ya Kanuni za Chama cha Kikomunisti cha China.