Rais wa Russia asema mlipuko wa Daraja la Crimea ni “shambulizi la kigaidi” lililopangwa na Ukraine
2022-10-10 09:04:31| CRI

Rais wa Russia Vladimir Putin amesema mlipuko wa Daraja la Crimea uliotokea jumamosi ulipangwa na kutekelezwa na Idara ya upelelezi ya Ukraine, na ni shambulizi la kigaidi lililofanywa dhidi ya miundombinu muhimu ya kiraia.

Rais Putin amesema hayo baada ya kusikiliza ripoti ya uchunguzi kuhusu mlipuko huo iliyotolewa na mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi ya Russia Alexander Bastrykin. Kwa mujibu wa ripoti hiyo njia ya usafiri wa gari lililolipuka, na washitakiwa waliopanga na kutekeleza mlipuko huo wamethibitishwa.

Gari moja lililipuka kwenye Daraja la Crimea na kusababisha kuwaka moto kwa mapipa saba ya mafuta yaliyokuwa kwenye treni iliyoendeshwa kwenye reli iliyoko kando ya barabara hiyo, ambapo watu watatu walikufa.

Wizara ya Ulinzi ya Ukraine ilithibitisha mlipuko huo kwenye mitandao ya kijamii lakini haikutoa maelezo zaidi.