Rais wa China ampongeza Van der Bellen kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Austria
2022-10-11 08:43:05| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Alexander Van der Bellen kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Austria.

Katika salamu zake, rais Xi amesema anatilia maanani sana uhusiano kati ya China na Austria, na yuko tayari kushirikiana na Bellen kusukuma mbele uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili ili kunufaisha nchi hizo na wananchi wao.