Jeshi la Somalia laua zaidi ya wapiganaji 200 wa kundi la al-Shabab
2022-10-11 08:43:33| CRI

Jeshi la Somalia limesema kuwa vikosi vyake vimeua zaidi ya wapiganaji 200 wa kundi la al-Shabab wakati wa operesheni iliyofanyika jumapili katika wilaya ya Bulaburte, katikati mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo, wapiganaji hao walikuwa wanapanga kuweka kizuizi katika barabara kati ya wilaya za Beledweyne na Bulaburke na kufanya shambulizi, lakini vikosi vya usalama vya Somalia vilipata taarifa za kiintelijensia kwa wakati mwafaka na kuzuia shambulizi hilo.

Jeshi la Somalia linaloungwa mkono na makundi ya wanamgambo wanaoikubali serikali ya nchi hiyo limekomboa zaidi ya vijiji 40 na kuua zaidi ya wapiganaji 500 wa kundi la al-Shabab katika wiki tatu zilizopita kwenye operesheni iliyofanyika katikati ya Somalia.