Makamu wa rais wa China kuhudhuria Mkutano wa Sita wa CICA
2022-10-11 20:41:44| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Mao Ning ametangaza kuwa, kutokana na mwaliko wa Serikali ya Kazakhstan ambayo ni Nchi Mwenyekiti wa Mkutano wa Hatua za Maingiliano na Kujenga Imani Barani Asia (CICA), makamu wa rais wa China Wang Qishan atahudhuria Mkutano wa Sita wa CICA utakaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 13 Oktoba, huko Astana.