Tanzania na Kenya zakubaliana kuongeza mapambano dhidi ya uhalifu wa kuvuka mipaka
2022-10-12 08:29:52| cri

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Kenya, William Ruto, jumatatu walikubaliana kuongeza mapambano dhidi ya uhalifu wa kuvuka mipaka, ikiwa ni pamoja na biashara haramu ya binadamu, ujangili na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Viongozi hao wawili pia wameahidi kuanzisha biashara kati ya nchi hizo mbili ili kupunguza umaskini na kuboresha ukuaji wa uchumi wa nchi hizo.