China yaunga mkono kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika
2022-10-12 08:34:20| cri

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing jana amesema, China inapongeza na kuunga mkono Umoja wa Mataifa kuimarisha zaidi ushirikiano na Umoja wa Afrika, ili kuhimiza zaidi maendeleo ya amani barani Afrika.

Balozi Dai amesema, bila kujali mabadiliko ya hali ya kimataifa, China siku zote inaunga mkono nchi za Afrika na Umoja wa Mataifa, na kutoa mchango zaidi kwa ajili ya kutimiza amani ya kudumu na maendeleo ya pamoja barani Afrika.