Ethiopia yathibitisha tarehe ya upigaji kura za maoni kuhusu kuongeza mkoa wa 12
2022-10-13 08:37:55| cri


 

Bodi ya Uchaguzi ya Ethiopia (NEBE) jana imetangaza kuwa imeweka tarehe 6 mwezi Desemba kuwa siku ya kupiga kura za maoni kuhusu kuongeza mkoa wa 12 nchini humo.

Mwezi Agosti, baraza la juu la bunge la Ethiopia lilipitisha azimio kuhusu kufanyika kwa upigaji kura za maoni kuhusu kuongeza mkoa wa 12 nchini humo.