China yapongeza Lesotho kwa kufanya uchaguzi wa wabunge kwa amani
2022-10-13 08:22:12| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Bibi Mao Ning jana amesema, China inaipongeza Lesotho kwa kufanikiwa kufanya uchaguzi wa wabunge kwa utulivu.

Hivi karibuni, matokeo ya uchaguzi wa wabunge nchini Lesotho yalitangazwa, ambapo chama kipya cha siasa cha Prosperity Revolution kilishinda karibu nusu ya viti vya bunge na kuwa chama kikubwa zaidi kinachotarajiwa kuunda baraza la mawaziri.