Mtaalamu wa Nigeria: Mkutano mkuu wa 20 wa CPC wabeba matarajio ya dunia
2022-10-13 14:43:27| CRI

Ni siku nyingine tunapokutana tena katika kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi cha leo tutakuwa na ripoti inayozungumzia Mkutano mkuu wa 20 wa CPC utakaofunguliwa Oktoba 16 hapa Beijing na jinsi unavyofuatiliwa kwa karibu na jamii ya kimataifa, na pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi kuhusu ubalozi wa China nchini Kenya kutoa ufadhili wa masomo kwa zaidi ya wanafunzi 20 wa Chuo Kikuu cha Nairobi, ikiwa ni katika kusherehekea miaka 73 tangu kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.