SIKU YA CHAKULA DUNIANI
2022-10-13 10:16:49| CRI

October 16 ya kila mwaka ni Siku ya Chakula Duniani. Siku hii inaadhimishwa ikiwa ni kuikumbusha jamii ya kimataifa kuwa, baa la njaa linaathiri kila mmoja wetu, awe tajiri ama masikini, katika nchi kubwa kiuchumi au nchi iliyo nyuma kiuchumi. Siku hii ni ilianzishwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, lengo kuu likiwa ni kupambana na njaa na kuboresha mifumo ya kilimo ili kuhakikisha baa la njaa linatokomezwa duniani.

Lakini dunia hivi sasa inakabiliwa na changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabianchi, ambayo yanachukua nafasi kubwa katika majanga ya kiasili kama vile mafuriko, ukame, na ongezeko kubwa la joto duniani. Nchi nyingi duniani kwa sasa zinakabiliwa na tatizo kubwa la ukame ama mafuriko, watu wanakimbia makazi yao kutafuta maji na chakula kwa ajili yao na mifugo yao, watoto, wa kike na wa kiume, wanaacha kuhudhuria shule na badala yake wanasaidia familia zao kuweza kujikimu kimaisha.

Katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake jumamosi ya leo, tutazungumzia Siku hii ya Chakula Duniani pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa wanawake na watoto.