Vijana barani Afrika watakiwa kuchukua nafasi za uongozi katika maendeleo ya bara hilo
2022-10-14 08:35:22| CRI

Vijana barani Afrika wamepewa changamoto ya kuchukua nafasi za uongozi na kuchukua nafasi muhimu katika ajenda ya maendeleo ya bara hilo.

Kauli hiyo imetolewa watu mbalimbali waliohutubia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa YouthConnekt Afrika ulioanza jana mjini Kigali, Rwanda. Mkutano huo wa siku mbili unaowaunganisha vijana kutoka ndani na nje ya bara hilo unafanyika chini ya kaulimbiu “Kuongeza kasi ya Uwekezaji kwa Vijana: Vijana Imara, Afrika Imara.”

Akizungumza kwenye hafla hiyo, rais wa Rwanda Paul Kagame amesema, vijana wanapaswa kuchukuliwa kama wenzi sawa katika ajenda za maendeleo za nchi husika.

Mada muhimu zitakazojadiliwa katika Mkutano huo wa siku mbili ni pamoja na mchango wa vijana katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi, amani na usalama endelevu, uvumbuzi katika sekta ya utamaduni na michezo.