Rais Xi Jinping aongoza mkutano wa wasio wanachama wa CPC ili kupata maoni kuhusu mkutano mkuu wa 20 wa Chama
2022-10-14 22:06:02| cri

Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ilifanya mkutano mwishoni mwa mwezi Agosti uliohudhuriwa na watu wasio wanachama mjini Beijing ili kusikiliza maoni na mapendekezo ya kamati kuu za vyama vingine vya siasa, mkuu wa Shirikisho la Viwanda na Biashara la China, na watu wasio na vyama kuhusu rasimu ya ripoti ya Kamati Kuu ya 19 ya CPC itakayotolewa kwenye mkutano mkuu wa 20 wa chama.

Xi Jinping, ambaye ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, aliongoza mkutano huo na kutoa hotuba muhimu, akisisitiza kuwa ili kukabiliana na majukumu na matakwa mapya yanayotokana na zama mpya na safari mpya, CPC na vyama vingine vya siasa lazima viimarishe ushirikiano, kuunganisha na kuendeleza umoja wa kizalendo, kuchangia busara na nguvu za watu kutoka pande zote, na kujitahidi kwa pamoja kujenga nchi ya kisasa ya ujamaa katika mambo yote na kufikia kuimarisha nguvu ya China.

Wajumbe waandamizi wa kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya CPC, wawakilishi wa vyama mbalimbali vya kisiasa, na wengine wengi walishiriki kwenye mkutano huo.