Madaktari wa China nchini Sierra Leone wasaidia katika mapambano dhidi ya Malaria
2022-10-14 08:34:38| CRI

Timu ya madaktari wa China nchini Sierra Leone wametoa mafunzo ya njia za kinga na tiba ya malaria kwa wafanyakazi wa afya katika Hospitali ya Urafiki ya China na Sierra Leone.

Mafunzo hayo yaliyotolewa na madaktari wa China jana, yalihusisha njia mbalimbali ikiwemo video fupi, na kazi halisi, na yalilenga kuboresha uwezo wa madaktari wa Sierra Leone katika kupambana na ugonjwa huo.

Mtaalamu wa maabara katika timu ya madaktari wa China, Zhan Xinjie, alitambulisha uelewa kuhusu ugonjwa huo na aina mbalimbali za vimelea vinavyosababisha malaria katika sehemu mbalimbali duniani, na kutoa mafunzo ya njia mpya za utambuzi wa kimaabara kwa wafayakazi wa afya wa nchini Sierra Leone.

Dokta Sallieu Kamara katika hospitali hiyo ameishukuru timu ya madaktari wa China kwa kuandaa mafunzo ya kina kwa wafanyakazi wa afya wa huko, akisema ufahamu mpya utasaidia katika kugundua mapema vijidudu vya malaria.