Bunge la Djibouti lalitangaza kundi la waasi kuwa la kigaidi
2022-10-14 08:34:52| cri


 

Bunge la Djibouti jana limelitangaza kundi la “Armed FRUD” kuwa kundi la kigaidi.

Uamuzi huo umekuja baada ya kundi hilo kushambulia kambi moja ya kijeshi kaskazini nchini humo na kusababisha vifo vya askari 7 na wengine 4 kujeruhiwa, na zaidi ya askari 6 hawajulikani walipo.

Shambulizi hilo limelaaniwa na mashirika ya kikanda na kimataifa, ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) na Ethiopia.