Makundi ya kisiasa ya Palestina yasaini makubaliano ya maridhiano mjini Algiers
2022-10-14 22:07:37| cri

Makundi 14 ya kisiasa za Palestina, zikiwemo Kundi la Fatah na Kundi la Hamas, jana, zilisaini makubaliano ya maridhiano katika mji mkuu wa Algeria, Algiers.

Makubaliano hayo yanayoitwa Azimio la Algiers, yanaeleza kuwa Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO) ndicho mwakilishi pekee halali wa watu wa Palestina.

Pia makundi hayo yamekubaliana kuchukua hatua halisi ili kufikia maridhiano ya kitaifa na kufanya uchaguzi mkuu ndani ya mwaka mmoja kuanzia tarehe ya kusainiwa kwa makubaliano hayo.