Tume ya Umoja wa Afrika yaweka mpango wa kusaidia polisi nchini Somalia kupambana na uhalifu
2022-10-14 08:37:13| CRI

Tume ya mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) imesema, kitengo cha Polisi katika Tume hiyo kimeandaa miongozo ya kusaidia Jeshi la Polisi la Somalia (SPF) kukamilisha mipango ya Polisi Jamii ili kupambana na uhalifu. 

Naibu Mratibu wa Mageuzi ya Polisi wa Tume hiyo Alex Ndili amesema, taratibu za kawaida za uendeshaji kuhusu Polisi Jamii zimeandaliwa kwa pamoja na Idara ya Polisi Jamii ya jeshi la Somalia ili kuimarisha hatua za kuzuia uhalifu.

Ndili amesema maendeleo ya taratibu hizo zitaunga mkono kuundwa kwa Polisi Jamii huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, na kwamba zimehusisha majukumu ya wadau mbalimbali katika polisi jamii, njia za kujulisha muundo wa Polisi Jamii, uundaji wa kamati mbalimbali na changamoto zinazokabili jamii.