Kenya yasema kampuni za China zimesaidia kuhimiza maendeleo ya viwanda nchini humo
2022-10-14 08:36:11| CRI

Kenya imesema wazalishaji wa China wanachukua nafasi chanya katika ajenda ya  kuhimiza maendeleo ya  viwanda nchini humo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Wanaviwanda la Kenya (KAM) Anthony Mwangi amesema, wanaviwanda wa China wameongeza vigezo vya ushindani nchini humo, na kuchochea maendeleo ya uvumbuzi zaidi nchini humo.

Amesema wanaviwanda kutoka China wanavutiwa na Kenya kwa kuwa nchi hiyo ni kitovu cha soko linalokua kwa kasi katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati. Ameongeza kuwa, wazalishaji wa kigeni walioko nchini Kenya wananufaika na miundombinu inayowawezesha kusafirisha bidhaa zao katika nchi nyingine za Afrika, na kwamba Kenya pia iko tayari kujifunza kutoka kwa China katika safari yake ya kuhimiza maendeleo ya  viwanda ambayo imeibadilisha nchi hiyo na kuwa nchi kubwa ya uzalishaji duniani.