Rais wa China atoa salamu za rambirambi kwa rais wa Nigeria kufuatia vifo vilivyotokana na ajali ya meli
2022-10-15 16:32:09| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za rambirambi kwa rais Muhammadu Buhari wa Nigeria kufuatia vifo vilivyotokana na ajali ya meli.

Rais Xi amesema ameshtushwa na habari kuhusu ajali ya meli iliyotokea kwenye Jimbo la Anambra, nchini Nigeria ambayo imesababisha vifo vya watu wengi. Kwa niaba ya serikali ya China na watu wake, ametoa salamu za pole kwa wahanga na kutoa salamu rambirambi kwa familia za ndugu wa waliokufa kwenye ajali hiyo.