Mkutano wa maandalizi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC wafanyika
2022-10-15 20:47:54| CRI

Mkutano wa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefanyika leo mchana kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, chini ya uenyekiti wa rais Xi Jinping.

Mkutano huo umepitisha ajenda ya Mkutano Mkuu wa 20 ambayo ni pamoja na kusikiliza na kukagua ripoti ya Kamati Kuu ya 19 ya Chama, kukagua ripoti ya kazi ya Kamati ya Ukaguzi wa Nidhamu ya Kamati Kuu ya 19, kukagua na kupitisha Marekebisho ya Katiba ya Chama cha Kikomunisti cha China, na kuunda Kamati Kuu ya 20 na Kamati ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu.