China daima haitafanya umwamba na kuvamia nchi nyingine
2022-10-16 12:34:45| CRI

Xi Jinping alipohutubia Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uliofunguliwa leo hapa Beijing amesema, China inafuata sera za kidiplomasia ambazo ni huria, za kujiamulia na za amani. Amesema siku zote China inaamua msimamo na sera zake kufuatia hali halisi, kulinda kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa na haki duniani, na inapinga kithabiti aina yoyote ya umwamba na siasa ya kinguvu, pia inapinga wazo la Vita Baridi, vitendo vya kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine, na kupinga vigezo viwili. Amesisitiza kuwa, China haitafanya umwamba, wala haitavamia nchi nyingine daima.