China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa nchi na sehemu zaidi ya 140
2022-10-16 12:32:23| CRI

Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefunguliwa leo mjini Beijing.

Xi Jinping amehutubia mkutano huo na kusema, China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa nchi na sehemu zaidi ya 140, na inashika nafasi ya kwanza duniani kwa thamani ya biashara ya bidhaa. Pia Xi amesema, China inashika nafasi ya kwanza katika kuvutia uwekezaji wa nje na kutoa uwekezaji kwa nchi za nje, na imeendeleza sera ya kufungua mlango kwa nje kwa upana na kina zaidi.