China kusukuma mbele lengo la kupunguza utoaji wa hewa chafu kwa hatua madhubuti na tulivu
2022-10-16 13:11:42| CRI

Xi Jinping alipohutubia Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uliofunguliwa leo hapa Beijing amesema, China itasukuma mbele kwa hatua madhubuti na tulivu kufika kilele cha utoaji wa hewa chafu na kutimiza usawa wa utoaji na ufyonzaji wa hewa hiyo. Pia amesema, China itashiriki kwenye usimamizi wa kimataifa wa juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.